Mwenda arejeshwa rasmi kikosini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Mwenda arejeshwa rasmi kikosini Yanga

Uongozi wa Yanga umesema suala la mchezaji Israel Patrick Mwenda limefikia mwisho baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kutoa uamuzi unaomtaka kurejea katika kituo chake cha kazi na kuzingatia adhabu pamoja na maelekezo yaliyotolewa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amesema klabu hiyo iliona umuhimu wa kuwasilisha suala la Mwenda katika kamati husika ili lipitiwe na kutolewa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani, Kamwe amesema kamati imekamilisha kazi yake na kwamba mchezaji huyo sasa anatarajiwa kurejea katika majukumu yake na kuendelea kutumikia mkataba wake na Yanga.

“Kwa mujibu wa taarifa ya kamati, mchezaji Israel Patrick Mwenda ameelekezwa kurejea katika kituo chake cha kazi, huku akitakiwa kuzingatia adhabu na maelekezo yaliyotolewa na kamati hiyo,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa uongozi wa klabu unatarajia Mwenda kuendelea kutoa mchango wake kwa timu na kuwapa furaha mashabiki kama ilivyokuwa ikitarajiwa kutoka kwake.

Kamwe amesema ameamua kutoa ufafanuzi huo kutokana na picha za mchezaji huyo kusambaa katika siku za hivi karibuni na kuzua maswali miongoni mwa mashabiki kuhusu hatma yake ndani ya klabu.

Amesisitiza kuwa suala hilo lilishughulikiwa kupitia utaratibu rasmi wa kamati husika na kwamba hatua inayofuata ni mchezaji kurejea kazini kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika uamuzi huo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Abuya nje wiki mbili
Abuya nje wiki mbili
2h ago
READ MORE β†’
Malengo yetu mbio za ubingwa Ligi Kuu yako palepale - Kamwe
Malengo yetu mbio za ubingwa Ligi Kuu yako palepale - Kamwe
2h ago
READ MORE β†’
Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa
Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa
5h ago
READ MORE β†’
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 13 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 13 2026
8h ago
READ MORE β†’
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
1d ago
READ MORE β†’
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
1d ago
READ MORE β†’
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
1d ago
READ MORE β†’