Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, ataendelea kusalia katika nafasi yake baada ya uongozi wa klabu hiyo kuridhia kutofanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa sasa.

Hatua hii imekuja kufuatia kuongezeka kwa shinikizo na joto la mashabiki kutaka mabadiliko ya benchi la ufundi baada ya Yanga kupoteza mchezo wa dabi ya Kariakoo kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Simba SC mnamo Oktoba 10, 2026.

Uamuzi wa uongozi wa Yanga unampa mwalimu huyo nafasi ya kujisahihisha kupitia michezo inayofuata, huku kukiwa na tathmini ya karibu juu ya mwenendo wa timu.

Michezo inayofuata ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA ya Madagascar inaweza kuamua hatma ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini hasa mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja wa Azam Complex.

Mabosi wa Yanga wamejiridhisha kupoteza mchezo dhidi ya Simba haitoshi kuwa sababu ya kumuondoa kocha huyo ambaye mechi yake ya kwanza dhidi ya Simba aliwaongoza Wananchi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutwaa Ngao ya Jamii.

Kwa sasa Yanga imeelekeza nguvu zake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa lengo likiwa kufuzu hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 13 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 13 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kamwe kufunguka mazito Jangwani Jumanne
Kamwe kufunguka mazito Jangwani Jumanne
15h ago
READ MORE β†’
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
22h ago
READ MORE β†’
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
23h ago
READ MORE β†’
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
1d ago
READ MORE β†’
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga itarejea ikiwa imara zaidi
Yanga itarejea ikiwa imara zaidi
1d ago
READ MORE β†’
Mabosi Yanga kufanya tathmini kipigo dhidi ya Simba
Mabosi Yanga kufanya tathmini kipigo dhidi ya Simba
2d ago
READ MORE β†’
Iweke Xtra 90 katika simu yako
Iweke Xtra 90 katika simu yako
2d ago
READ MORE β†’