Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'

Beki wa kulia wa Yanga, Yao Kouassi Attohoula, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutoikatia tamaa timu yao, huku akiwaomba kudumisha umoja na mshikamano kufuatia kipigo cha kwanza cha msimu walichokipata kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba SC.

Yanga walipoteza mchezo huo wa Dabi ya Kariakoo kwa kufungwa Mabao 2-1 dhidi ya Simba SC katika mchezo uliopigwa siku ya Jumamosi, Oktoba 10, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yalisitisha rekodi ya Yanga ya kushinda mechi zote sita za kwanza za Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

Kupitia ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Yao alikiri kuwa matokeo hayo yameleta maumivu makubwa lakini akasisitiza kuwa ni sehemu ya mchezo wa soka na sasa akili zao zote zimeelekezwa katika kujiimarisha na kuwa bora zaidi.

“Kushindwa kunauma, lakini ni sehemu ya mchezo. Jana imepita, tumekubali makosa yetu mbalimbali ili tujifunze na kufanya vizuri zaidi. Tusikate tamaa maadamu bado tunapumua. Tuendelee kuwa kitu kimoja, tushikamane na kupambana pamoja,” alisema Yao.

Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kurejea mazoezini kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CFFA utakaopigwa Jumamosi Oktoba 17 kwenye uwanja wa Azam Complex.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
13m ago
READ MORE β†’
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
1h ago
READ MORE β†’
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 12 2026
6h ago
READ MORE β†’
Yanga itarejea ikiwa imara zaidi
Yanga itarejea ikiwa imara zaidi
20h ago
READ MORE β†’
Mabosi Yanga kufanya tathmini kipigo dhidi ya Simba
Mabosi Yanga kufanya tathmini kipigo dhidi ya Simba
1d ago
READ MORE β†’
Kuumia kwa Abuya kulitugharimu - Manqoba
Kuumia kwa Abuya kulitugharimu - Manqoba
1d ago
READ MORE β†’
Mchezo dhidi ya TRA United kupangiwa tarehe nyingine
Mchezo dhidi ya TRA United kupangiwa tarehe nyingine
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 2-1 Yanga, Ligi Kuu (FT)
Highlights; Simba 2-1 Yanga, Ligi Kuu (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 11 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 11 2026
1d ago
READ MORE β†’