Manqoba aweka mkakati wa kuidhibiti Simba Kariakoo Derby

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2026
Manqoba aweka mkakati wa kuidhibiti Simba Kariakoo Derby

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, ameweka wazi kuwa mipira ya kutenga na adhabu (set pieces) ndiyo silaha hatari zaidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo unaosubiriwa kwa hamu nchini.

Katika maandalizi ya mwisho kuelekea dabi hiyo ya Ligi Kuu ya NBC itakayopigwa kesho, Jumamosi, Oktoba 10, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru, Mngqithi amefichua kuwa ameshasuka mkakati thabiti wa kuwazima wapinzani wao na kuhakikisha wanaondoka na alama tatu muhimu.

Akizungumza kuhusu uchambuzi wake kuelekea mchezo huo, Mngqithi alibainisha kuwa Simba ina faida kubwa ya wachezaji wenye miili mirefu na uwezo mkubwa wa kuruka, jambo linalowafanya kuwa hatari inapofika kwenye matumizi ya kona na faulo karibu na lango.

Kocha huyo aliwataja walinzi na mshambuliaji Ibrahim Doumbia, Rushine De Reuck, na Ismail Toure, kama wachezaji wa kuchungwa zaidi kutokana na hatari yao kwenye mipira ya juu.

"Tumechambua kwa umakini jinsi wanavyocheza. Ni timu hatari sana kwenye mipira ya adhabu na kona kwa sababu wana wachezaji warefu na wenye nguvu kama Doumbia, De Reuck, na Toure."

"Tumefanya maandalizi kwa kuzingatia ubora na nguvu yao, hasa katika mipira ya adhabu na kona, tutahitaji kuwazuia wasifike eneo la hatari karibu na lango letu," alisema.

Mngqithi aliongeza kuwa anawafahamu vizuri baadhi ya wachezaji wa Simba kwa kuwa amewahi kufanya nao kazi huko nyuma, jambo linalompa mwanga wa jinsi ya kuwadhibiti.

Nae Mshambuliaji Selemani Mwalimu, amemtaja Peter Shalulile kuwa mchezaji mwenye uzoefu ambaye wachezaji wenzake wanajifunza mengi kutoka kwake, akieleza kuwa wana imani naye kuelekea Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC.

Mwalimu amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kesho, Jumamosi, Oktoba 10, kwenye Uwanja wa Uhuru, ili kuwapa nguvu wachezaji. Amesema kikosi kimejiandaa vizuri na kila mchezaji atakayepata nafasi atapambana kwa ajili ya nembo ya timu.

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
1h ago
READ MORE β†’
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
3h ago
READ MORE β†’
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
3h ago
READ MORE β†’
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
10h ago
READ MORE β†’
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
11h ago
READ MORE β†’
Dube aipa ubingwa wa kihistoria Hardrock FC
Dube aipa ubingwa wa kihistoria Hardrock FC
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar kutoka Moshi
Yanga yarejea Dar kutoka Moshi
2d ago
READ MORE β†’