Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wako uwanjani KMC Complex kuwakaribisha Pamba Jiji katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC mchezo wa raundi ya nne.
Baada ya kugawa vipigo katika mechi ziizopita, Wananchi watashuka dimba la KMC Complex wakiwa na dhamira ileile, kuendelea kugawa dozi na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi.
Hata hivyo wanakutana na Pamba Jiji inayoonolewa na kocha Francis Baraza aliyejipambanua kwa uwezo wake wa kujenga timu zinazojilinda vyema.
Licha ya uimara huo, leo watahitaji kuwa kwenye ubora mkubwa kuwadhihiti Yanga ambao katika mechi tatu zilizopita wamefunga mabao 11.
Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngqithi ameunda kikosi kinachocheza soka la kushambulia mda wote wakiwanyima wapinzani nafasi ya kupumua.
Mpaka sasa Yanga ndo vinara wa kuzifumania nyavu msimu huu, Peter Shalulile, Maxi Nzengeli, Albert Kangwanda na Chadrack Boka wakiwa vinara wa kuzifumania nyavu kila mmoka akiweka kambani mabao mawili.
Aidha leo huo mashabiki wa Yanga wakamshuhudia mshambuliaji Suleiman Mwalimu ambaye sasa yuko tayari kuanza kutumika baada ya taratibu zote za usajili wake kukamilika kwa asilimia 100.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 3 usiku. Matokeo ya ushindi yatairejesha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi