Matchday; Yanga vs Azam Fc, Muungano Cup, SF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Apr 2026
Matchday; Yanga vs Azam Fc, Muungano Cup, SF

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo watashuka dimba la New Amaan Complex kuikabili Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali kombe la Muungano.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini, utapigwa saa 2:15 ukizikutanisha timu mbili zenye upinzani wa aina yake.

Yanga ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo na leo watashuka dimbani kwa lengo la kusaka ushindi ili kufuzu hatua ya fainali.

Hata hivyo haitakuwa mechi rahisi kwani wanakutana na Azam Fc ambayo inaona michuano hii inaweza kuwapa nafasi ya kutinga fainali ili kuwania taji lao la kwanza chini ya kocha Florent Ibenge.

Mpaka sasa unaweza kusema nafasi ya Azam Fc kutwaa ubingwa wa ligi kuu ni ndogo kwani wamezidiwa alama 10 na vinara wa ligi hiyo Yanga hivyo kwao mechi hii ina umuhimu mkubwa kwani ni njia mbadala kwao kushinda taji.

Kwa Yanga ni mchezo wa kulinda heshima ya klabu kwani licha ya kukabiliwa na mchezo mgumu wa dabi ya Kariakoo siku chache zijazo, Yanga imepania kufuzu fainali ili kutetea taji hilo kabla ya kuelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Simba utakaopigwa May 03 katika uwanja wa Isamuhyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’