FT : Yanga 3-0 Prisons, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2026
FT : Yanga 3-0 Prisons, NBC PL

Dakika 45 za kipindi cha pili zimetosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Licha ya kutawala mchezo dakika 45 za kipindi cha kwanza, Tanzania Prisons walifanikiwa kukabiliana na presha ya mashambulizi mfululizo na kwenda mapumziko wakiwa hawajafungwa.

Hata hivyo kipindi cha pili Yanga ilibadili mbinu za mashambulizi ikipitisha mipira pembeni.

Alikuwa na Allan Okello 'Star Boy' akifungua kalamu ya mabao kwenye dakika ya 50 akimalizia krosi ya Israel Mwenda.

Baada ya Yanga kufunga bao hilo mechi ilifunguka zaidi Tanzania Prisons wakijaaribu kusogea juu kusaka bao la kusawazisha.

Hapo ndipo Wananchi wakapata nafasi ya kuongeza bao la pili kupitia Mudathir Yahya aliyemalizia pasi ya Allan Okello katika dakika ya 68 kabla ya Pacome Zouzoua ambaye mapema alifunga bao lililokataliwa na mwamuzi msaidizi kwa kigezo cha kuotea, kafunga bao la tatu dakika ya 86 akimramba chenga mlinda lango wa Prinsons Moussa Mbissa baada ya kuwahi pasi mpenyezo iliyowekwa na Duke Abuya.

Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ambao zinamaliza ukame wa Wananchi kupata ushindi baada ya dakika 270.

Yanga imejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 41.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’