FT : Yanga 3-0 JS Kabylie, CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2026
FT : Yanga 3-0 JS Kabylie, CAFCL

Yanga imemaliza kibabe hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikiifumua JS Kabylie mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex.

Unaweza kusema vijana wa kocha Pedro Goncalves hawana deni kwani leo walipambana tangu dakika ya kwanza kusaka ushindi huo na pengine mechi ilipaswa kuisha kwa Yanga kufunga mabao mengi zaidi.

Alikuwa ni Pacome Zouzoua aliyetengeneza nafasi ya bao la kwanza baada ya kufanyiwa madhambi eneo la hatari na mwamuzi Jacques Ndala kuamuru mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Depu.

Hata hivyo Pacome alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mudathir Yahya.

Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 wakirejea kipindi cha pili wakiwa na ari kubwa zaidi na kufanikiwa kufunga mabao mwengine mawili kupitia kwa Depu na Chadrack Boka.

Ni ushindi ambao hata hivyo haujatosha kuipeleka Yanga robo fainali baada ya mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya AS FAR kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

Yanga imemaliza nafasi ya tatu kundi B ikifikisha alama nane huku AS FAR wakimaliza nafasi ya pili na alama 9, Al Ahly wakiongoza kundi na alama 10.

Matokeo ya mchezo dhidi ya Al Ahly uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 nyumbani unaweza kusema ndio yaliyovuruga hesabu za Yanga kutinga robo fainali.

Lakini ni wazi Yanga imepambana katika kundi gumu, na sasa inapaswa kuendeleza kasi hii kwenye mashindano ya ndani ili kuhakikisha inashinda kila taji.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’