Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga watashuka dimba la KMC Complex kuikabili Mashujaa Fc.
Utakuwa mchezo wa kwanza wa ligi kwa Yanga mwaka huu 2026 Wananchi wakipania kuendeleza rekodi nzuri waliyomaliza nayo mwaka 2025.
Ushindi utaihakikishia Yanga kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi na kuongeza gap la pointi dhidi ya watani zao Simba ambao jana walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Katika mchezo huo huenda mashabiki wa Yanga wakapata nafasi ya kuwashuhudia mastaa wao wapya Mohamed Damaro Camara, Allan Okello, Emmanuel Mwanengo na hata Depu ambao walikuwa sehemu ya kikosi kilichokamilisha maandalizi jana kuelekea mchezo huo.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves atautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Ijumaa ya wiki hii huko Misri.