Yang imetinga nusu fainali ya kombe la Mapinduzi kibabe baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TRA United katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex.
Bao pekee la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na Ecua Celestin akimalizia pasi ya Maxi Nzengeli.
TRA United waliipa Yanga upinzani mkali wakihimili mikiki mikiki ya mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
TRA United walipata nafasi kadhaa dakika za lala salama lakini uimara wa mlinda lango Aboutwalib Mshery na safu ya ulinzi ya Yanga uliwahakikishia Wananchi ushindi huo.
Yanga sasa itachuana na Singida BS kwenye mchezo wa nusu fainali Januari 09.

ADVERTISE HERE