Yanga imeanza vibaya mechi ya mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika ikikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Silver Strikers huko Malawi
Bao la Yosefe kwenye kipindi cha pili liliizamisha Yanga ilioanza mchezo huo taratibu huku ikitengeneza mashambulizi machache katika lango la wapinzani wao
Yanga ilizindua baada ya kuingia kwa bao hilo lakini unaweza kusema muda haukutosha kurejea mchezoni kwani wapinzani wao walitumia kila mbinu ikiwa ni pamoja na kupoteza muda ili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo nyumbani
Yanga ina dakika 90 nyumbani kupindua matokeo hayo ikihitaji ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kutinga hatua ya makundi
Ni wazi mechi ya mkondo wa pili itakayopigwa Oktoba 25 itakuwa Do or Die kwa Yanga