Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kiungo wa Yanga Salum Abubakar 'Sureboy' au Babu Kaju
Tangu ajiunge na Yanga akitokea klabu ya Azam Fc, Sure Boy ameendelea kuwa mchezaji maalum katika kikosi cha Wananchi
Mwenyewe hupenda kujiita 'kuni ya akiba' kwani unaweza usimuonea katika mechi nyingi lakini siku ukimuona kikosini utabaini thamani yake
Mkumbuke Sure Boy wa mechi za kombe la Shirikisho misimu mitatu nyuma dhidi ya Club Africain pale Tunisia au fainali ya pili CAF CC dhidi ya USM Alger kule Algeria
Katika fainali hiyo aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi aliwakosa viungo wake tegemeo Yannick Bangala na Khalid Aucho lakini Sureboy akachukua jukumu la kucheza eneo la kati huku akisaidiana na Mudathir Yahya, Yanga ikishinda bao 1-0 katika mchezo uliokuwa na presha kubwa
Wananchi wataendelea kumuona Sureboy katika kikosi cha Yanga kwa msimu mwingine tena
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa
HAPPY BIRTHDAY BABU KAJU...!