Yanga imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo baada ya kuichapa Prisons mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine, Mbeya
Yanga ililazimika kusubiri kwa takribani dakika 30 kuhesabu bao la kwanza kupitia kwa Mudathir Yahya aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Israel Mwenda
Kuingia kwa bao hilo ni kama kulifungua lango ya Prisons kwani Clatous Chama aliongeza bao la pili dakika chache kabla ya mapumziko akimalizia pasi ya Clement Mzize
Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala mchezo na kuongeza mabao mengine matatu yaliyofungwa na Israel Mwenda na Pacome Zouzoua aliyepachika mabao mawili
Yanga ilipata pigo pale mshambuliaji Prince Dube alipopata changamoto ya maumivu ya misuli ya nyuma ya paja mapema katika kipindi cha kwanza lakini nafas yake ilichukuliwa na Chama aliyefunga bao muda mfupi baada ya kuingia
Ulikuwa mchezo ambao pengine Yanga ingefunga mabao zaidi Chama, Mzize na Pacome wakikosa nafasi nyingine za wazi
Pacome aliyeibuka nyota wa mchezo huo, sasa amefikisha mabao 11 akisogea juu katika vita ya ufungaji bora
Yanga imefikisha alama 76 ikiendelea kusalia juu ya msimamo licha ya watani zao Simba nao kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KenGold





