Matchday : Kagera Sugar vs Yanga, NBC PL, Aug 29

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2024
Matchday : Kagera Sugar vs Yanga, NBC PL, Aug 29

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga leo wanaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa nne mfululizo ligi kuu ya NBC kwa kuikabili Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba

Mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini, utapigwa kuanzia saa 11 jioni

Mabadiliko ya muda wa mchezo huo yalithibitishwa na Bodi ya Ligi jana baada ya maombi ya Azam TV ili kuhakikisha mashabiki watakaofuatilia mchezo huo kupitia televisheni wanapata picha bora

Yanga ilitua Kagera jana na jioni vijana wa kocha Miguel Gamondi wakapata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Kaitaba

Ni wazi itakuwa mechi ngumu yenye upinzani mkali kwani Kagera Sugar hawajawahi kuwa wapinzani wepesi wanapocheza na Yanga hasa katika uwanja wa Kaitaba

Katika mchezo huo Yanga itawakosa wachezaji Yao Kouassi na Farid Mussa ambao ni majeruhi huku kiungo Khalid Aucho akirejea baada ya kupona changamoto ya misuli

Ni mwanzo wa msimu mwingine kwa Yanga, Wananchi wakiwa na matarajio makubwa kwa timu yao ambayo tayari imeonyesha ubora mkubwa kuanzia pre-season, Ngao ya Jamii na mechi za awali ligi ya mabingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’