Hawa ndio wapinzani wa Yanga, Zalan Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2022
Hawa ndio wapinzani wa Yanga, Zalan Fc

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Klabu ya Yanga itaanza kampeni yake kwenye hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza na Zalan FC ya Sudan ya Kusini.

Yanga itaanzia ugenini kwa mchezo wa kwanza utakaopigwa kati ya Septemba 9 hadi 11 huku marudiano ikichezwa kati ya Septemba 16 hadi 18.

Mshindi wa jumla baina ya klabu hizo atacheza na mshindi kati ya Mabingwa wa Ligi ya Ethiopia St. George au Al Hilal ya Sudan.

Zalan ambao ni mabingwa wa Ligi ya Sudan Kusini huenda ikatumia uwanja wa Al Hilal katika mechi zake za kimataifa kutokana Sudan Kusin kutokuwa na uwanja ambao unakidhi vigezo vya CAF.

Wametokea katika mji wa Rumbek uliopo katikati mwa nchi ya Sudan Kusini, ilianzishwa 1999 na wapinzani wao kwenye mashindano Yanga iliyoanzishwa 1935.

Zalan inashiriki kwenye ligi ya Sudan ambayo kutokana na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe imekuwa ikisimamiwa chini ya uangalizi wa Serikali.

Timu hiyo ilitwaa ubingwa na kujikatia tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara yake ya kwanza tangu 1999 ilipoanzishwa

Zalan walishinda ubingwa wa ligi kuu ya Sudan Kusini kwa mara ya kwanza msimu wa 2021/22 na kushinda pia Kombe la Shirikisho 2018.

walimaliza nafasi ya pili kwenye kundi B mwaka 2017 ilipofungwa na Gonzaga mabao 4-2 kwenye ligi ya Sudan (the South Sudan national league ‘SSNL’) mjini Juba kabla ya kutwaa ubingwa 2018 kwa kuifunga Gold Star mabao 4-0.

Msimu wa kwanza wa ligi hiyo ulikuwa 2013 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Sudani Kusini kutangaza kupata uhuru wake

Sio timu yenye historia na mafanikio makubwa lakini hata hivyo Yanga haipaswi 'kuwachukulia poa'

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’