Yanga walikuwa bora dhidi ya Ken Gold, tatizo ni matumizi ya nafasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Feb 2021
Yanga walikuwa bora dhidi ya Ken Gold, tatizo ni matumizi ya nafasi

Katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Ken Gold ambao ulipigwa uwanja wa Uhuru jana, ukiangalia takwimu za mchezo huo, unaweza ushangazwe na lawama zinazotolewa na baadhi ya mashabiki wa Yanga kuwa timu yao ilicheza chini ya kiwango

Takwimu za Azam zinaonyesha Yanga ilimiliki mchezo kwa asilimia 68, jumla ya mashuti 17 yalipigwa langoni kwa Ken Gold, mashuti nane yakilenga goli ukilinganisha na mashuti manne yaliyopigwa na Ken Gold, mawili yakilenga goli

Yanga ilipiga kona 16 dhidi ya kona tano zilizopigwa na Ken Gold

Yanga ndio timu iliyokuwa akisaka ushindi kwenye mchezo huo wakati Ken Gold walipaki basi kwa muda mwingi na kutumia mashambulizi ya kushitukiza

Kidogo Carlinhos alipotolewa nje kwa kadi nyekundu ndio wakajaribu kufunguka

Pengine hii ndio mechi ya kwanza Yanga imetengeneza idadi kubwa ya nafasi lakini wakatumia moja kupitia mkwaju wa penati

Lakini pia kama waamuzi wangekuwa waungwana, Yanga ingeweza kupewa mikwaju mitatu ya penati kwani kabla ya Fiston kufunga kulikuwa na matukio mengine mawili ya wachezaji wa Ken Gold kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Ukiwaangalia Yanga, utagundua ipo kazi imefanyika, changamoto ya kufunga mabao naamini itapatiwa majibu karibuni kwani timu imeanza kutengeneza nafasi nyingi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’