Ili kuhakikisha Yanga inasonga mbele hatua inayofuata michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mabosi wa Yanga wamesema tayari wamepata taarifa muhimu za 'kuwamaliza' wapinzani wao katika mechi ya mzunguko wanne wa mashindano ya Kombe la FA, Kengold FC ya jijini Mbeya
Yanga itawakaribisha Kengold katika mechi ya michuano hiyo itakayochezwa Jumaosi kwenye Uwanja wa Uhuru
Mkurugenzi wa Mashindano Thabit Kandoro amebainisha kuwa wameifuatilia Kengold kiufundi na ripoti kumkabidhi kocha Cedric Kaze.
"Hatutadharau timu yoyote ambayo tunakutana nayo, Kengold FC sio timu ya kuibeza, tumewafuatilia na taarifa zao tumeziwasilisha kwenye benchi la ufundi ili kufanyiwa kazi," alisema Kandoro
Kiongozi huyo aliongeza Yanga imejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika
Baada ya mchezo huo Yanga itasafiri mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikianzia mkoani Tanga ambako March 04 watcheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union kisha kuelekea kule Moshi kuifuata Polisi Tanzania