Shikhalo awashukia wanaomzushia kuhamia Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2021
Shikhalo awashukia wanaomzushia kuhamia Simba

Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo ameeleza kushangazwa na taarifa zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefanya mazungumzo na Simba ili ajiunge nao mkataba wake utakapomalizika na Yanga mwishoni mwa msimu

Mkenya huyo aliyeonyesha umahiri langoni katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, amesema hajafanya mahojiano na chombo chochote cha habari hivyo taarifa hizo ni uzushi wa mitandaoni

Amesisitiza kuwa yeye ni mchezaji wa Yanga, bado ana mkataba na mabingwa hao wa kihistoria na anaheshimu mkataba wake

"Ninapenda kuomba radhi juu ya taarifa zinazoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa kuna mazungumzo nimefanya nao kuhusu mkataba wangu na taarifa za mazungumzo na baadhi ya timu"

"Naomba nikanushe kuwa sikufanya mazungumzo na kituo chochote cha radio wala timu yoyote Mimi ni mchezaji wa Yanga na bado ninamkataba nao na nawaheshimu wajiri wangu," amefunguka Shikhalo

Taarifa iliyoenea mtandaoni, imebainisha kuwa mtangazaji wa eFM Sudi Mkumba ndiye aliyedai kuwa kipa huyo wa Kimataifa ambaye hudakia Harambee Stars atahamia Simba mwishoni mwa msimu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’