Carlinhos amtumia salamu Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Feb 2021
Carlinhos amtumia salamu Kaze

Carlos Carlinhos jana aliwapa furaha mashabiki wa Yanga akifunga bao muhimu lililoihakikishia Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar

Ni ushindi ambao umewafanya Wananchi wazidi kujichimbia kileleni wakifikisha alama 49, alama saba dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili

Carlinhos alihitaji dakika 20 tu kufanya mambo adimu ambayo yalikosekana katika dakika 70 kabla ya yeye kuingia

Mikimbio yake ilikuwa changamoto kwa mlinzi wa kulia wa Mtibwa Sugar Hassan Kessy ambaye mara kadhaa alijikuta akiramba nyasi huku Carlinhos 'akisepa' na gozi la n'gombe

Alipoweka bao kambani, Carlinhos hakushangilia, bila shaka ilikuwa ujumbe kwa kocha Cedric Kaze kuwa anataka muda zaidi wa kucheza

Pengine benchi la ufundi linahofia kumtumia muda mrefu kwani ametoka katika majeraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya miezi mitatu

Lakini Carlinhos ni mchezaji aliyekamilika sana kiufundi, huyu unaweza kumuweka daraja moja na Saido Ntibazonkiza

Katika michezo sita aliyoanza kwenye kikosi cha Yanga, Carlinhos amehusika kwenye mabao matano, akifunga mabao matatu na kutoa pasi za mabao mawili

Kwa namna yoyote kama yuko kwenye afya nzuri, Kocha Cedric Kaze anakosa sababu ya kutomtumia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’