Lwandamina haidharau St Louis

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Dec 2017
Lwandamina haidharau St Louis
Baada ya kuwafahamu wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha wa klabu ya Yanga George Lwandamina amesema hawezi kuidharau timu hiyo ya Shelisheli, na kitu cha msingi atahakikisha wanafanya maandalizi yakutosha ili waweze kuwa na uhakika wa matokeo.

Yanga imepangwa kuanza na St Luis ya Shelisheli na kocha huyo raia wa Zambia ameiambia Goal, hawezi kujihakikishia ushindi kwasababu hawajui wapinzani wao hivyo njia pekee ya kuwa na uhakika ni kujiandaa vizuri ndani ya uwanja.

"Mchezo wa soka umekuwa sana unaweza kuizarau St Luis kwasababu wapo Shelisheli, lakini kila kunapokucha mchezo wa soka unapiga hatua hakuna timu dhaifu ambayo unaweza kuingia uwanjani ukawa na uhakika wa kupata matokeo zaidi ya kufanya maandalizi ya mazuri ambayo naamini ndiyo yanaweza kukupa kile unachokitaka," amesema Lwandamina.

Kocha huyo amesema malengo yake ni kutaka Yanga iweze kucheza hatua ya makundi safari hii hivyo atazitimia mechi za ligi pamoja na michuano ya Kombe la Mapinduzi pamoja na FA, ili kukiimarisha kikosi chake na hatimaye kupata kile ambacho amekikusudia pamoja na jeshi lake.

Mzambia huyo amesema anajua siyo kazi nyepesi kufikia malengo hayo, lakini amepanga kuwa mkali kwa wachezaji wote watakaoonyesha uvivu kwenye mazoezi ili kila mmoja aweze kutoa mchango wake na hatimaye kuweza kufikia kile walichokikusudia msimu huu.

Yanga hawakuwa na wakati mzuri msimu uliopita baada ya kutolewa mapema kwenye michuano hiyo, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Zanaco FC na katika mchezo wa marudiano timu hizo ziligawana tena pointi kwa kucheza bila kufungana.

GOAL
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’