Nani aanze, nani asubiri vs Mtibwa Sugar leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Feb 2021
Nani aanze, nani asubiri vs Mtibwa Sugar leo?

Ukiwaondoa Saido Ntibazonkiza na Yacouba Songne ambaye pamoja na kuanza mazoezi bado hajawa fiti, kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze leo atakuwa na kikosi chake kamili wakati atakapoikabili Mtibwa Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mabadiliko pekee yanayoweza kushuhudiwa leo ni katika eneo la ushambuliaji ambalo ndilo linaloonekana kuwa na changamoto zaidi

Fiston Abdul Razak anaweza kurejeshwa kikosini kuongeza nguvu katika eneo hilo ambalo pia Ditram Nchimbi anaweza akapewa nafasi ya kuanza mbele ya Michael Sarpong

Nchimbi amekuwa na faida ya 'ku-press' walinzi wa timu pinzani pamoja na kuwa umakini wake ni mdogo katika kutumia nafasi kupachika mabao

Deus Kaseke aliyefunga mabao sita, ndiye anayetizamwa zaidi kuendelea kuifungia Yanga mabao

Kaseke amekuwa na kiwango kizuri sana msimu huu akisahihisha makosa ya safu ya ushambuliaji kwa kufunga mabao kila anapopata nafasi

Carlos Carlinhos alikosa mchezo uliopita, pengine leo anaweza kuwa na dakika zake

Umuhimu wa Carlinhos unafahamika hasa kwa mipira ya adhabu. Tangu apone majeraha Kaze hamtumii sana katika kikosi chake

Lakini kwa timu inayohitaji ushindi, Carlinhos ni mchezaji muhimu kwani anaweza kuifanya mipira ya kona na adhabu kuwa nafasi adimu zinazoweza kuipa Yanga mabao

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulipigwa mkoani Morogoro, mpira wa kona wa Carlinhos ndio uliozaa bao pekee la Yanga lililofungwa na nahodha Lamine Moro

Msimu huu amefunga mabao mawili na kutengeneza mabao mawili katika mechi alizocheza mwanzoni mwa msimu kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu

Ni mchezo ambao kocha Cedric Kaze anapaswa kuchanga karata zake vyema kuhakikisha timu yake inaweza kupata ushindi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’