Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 16, 2021 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi Kuu na kufanya maamuzi mbalimbali
Klabu ya Yanga imepigwa faini ya jumla ya Tsh Milioni Moja kutokana na makosa yaliyofanyika katika mechi dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City
Katika mchezo dhidi ya Prisons Yanga imepigwa fainli ya Tsh laki tano baada ya mashabiki kuonekana wakimwaga kimiminika katika maeneo ambayo wachezaji walikuwa wakipita baada ya kuteremka kwenye basi wakielekea vyumbani. Tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina
Aidha taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza kuwa katika mchezo dhidi ya Mbeya City, Yanga imepigwa faini ya Tsh Laki Tano baada ya mashabiki kuwatupia chupa waamuzi baada ya mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
