Miaka 86 ya klabu ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2021
Miaka 86 ya klabu ya Yanga

Ilipoanzishwa 1935 Klabu ya Yanga, makao makuu ya Klabu yalikua kwenye nyumba ya kupanga

Mwaka 1963 uongozi wa Mzee Mohamed Sultani (Mobosti) - Mwenyekiti, Mzee Kitwana Kondo Makamu na Mzee Jabir Katundu akiwa Katibu Mkuu walikuja na wazo la Yanga kuwa na jengo lake.

Mwaka 1964 Viongozi hao waliandaa mchezo wa kirafiki na Klabu ya Abaluhya (FC Leopards) ambayo ilikua imeanzishwa mwaka huo, na kwenye mchezo huo wa kirafiki Yanga ilifanikiwa kupata Tsh. 13,000/=, hela ambayo ilitosha kabisa kununua Jengo la Mafia lililopo mtaa wa Mafia na Nyamwezi hivyo kuwa Klabu ya Kwanza kuwa na jengo lake ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Mwaka 1969 viongozi waliona kuwa Yanga inahitaji Makao Makuu yenye hadhi zaidi ya waliokuwa nayo, hivyo kuamua kufunga safari kwenda kwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume kumuomba ufadhili, lakini mzee Karume alitoa sharti moja, kwamba lazima Viongozi wa Yanga waambatane na Viongozi wa Queens FC (Simba kwa sasa) watakapoenda kumuona, na walifanya hivyo.

Baada ya kupewa wazo hilo, Mzee Karume alikubali kujenga jengo moja ambalo litamilikiwa na vilabu vyote viwili, lakini wazo hilo liligonga mwamba, ndipo aliamua kuipa Yanga Tsh. 2,000,000/= ili wakajenge jengo lao, Kupitia kwa Mzee Rashid Kawawa, Mzee Karume aliwakabidhi hundi hiyo Mzee Mangara na Mzee Ramadhani Mwinyikambi.

Viongozi wa Yanga kwa kushirikiana na Wajerumani waliweza kupata mchoro na mkandarasi wa kujenga jengo la Jangwani kwa Tsh. 800,000/=.

Walivyopeleka michoro hiyo City Council kwa ajili ya kuidhinishwa, Injinia mmoja aliyefahamika kwa jina la Lunyasi aliyekuwa mwanachama wa Simba alikataa kupitisha mchoro huo kwa madai kwamba eneo lile ni jalala likijengwa jengo litaanguka.

Viongozi walimfikishia taarifa hiyo Mzee Karume ambaye alifunga safari kuja mpaka Jangwani kuweka jiwe la msingi na kuruhusu ujenzi kuanza mala moja

Jengo la Yanga ni moja ya urithi wa asili (natural heritagate) hivyo kila mwana Yanga hana budi kulilinda na kulitunza kwa gharama yoyote ile

Mungu ibariki Yanga, Mungu wabariki wana Yanga.

Makala hii imeandikwa na Simon Patrick aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’