Mukoko awapa somo washambuliaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Feb 2021
Mukoko awapa somo washambuliaji Yanga

Kiungo wa Yanga Mcongomani Mukoko Tonombe amesema ni jukumu lao wachezaji kuhakikisha wanashinda mechi na kutimiza malengo yao ya msimu huu

Mukoko ambaye juzi alionyesha kukerwa na waamuzi wa mchezo dhidi ya Mbeya City, amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto ya waamuzi akitolea mfano wa kunyimwa penati ya wazi, amesisitiza ni muhimu wao wachezaji kuhakikisha wanatumia nafasi nyingi wanazotengeneza

"Ni jukumu letu sisi wachezaji kuhakikisha tunashinda ili kuwapa furaha mashabiki. Tunapaswa kuongeza umakini hasa kwa safu ya ushambuliaji tutumie vyema nafasi tunazotengeneza"

"Tunapoteza nafasi nyingi sana, tukizitumia nafasi hizo hatuwezi kukosa ushindi hata inapotokea waamuzi wakatukwamisha. Ili mashabiki wetu wafurahi tunapaswa kushinda mechi. Tukiwa tunafunga mabao mengi hata timu pinzani tutakuwa tunazipunguza nguvu" alisema Mukoko

Vinara hao wa ligi kuu watakuwa na nafasi ya kusahihisha makosa keshokutwa Jumatano wakati watakaposhuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa kukata na shoka

Huu ni mchezo ambao matokeo tofauti na ushindi yataweza kuwaongezea presha wachezaji na benchi la ufundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’