Beki kisiki wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amerejea kikosini kuendelea na majukumu yake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa mkoani Mbeya Jumamosi, Februari 13, 2021
Mwamnyeto ambaye pia ni nahodha msaidizi wa Yanga, alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa nchini Cameroon ambako walishiriki michuano ya CHAN
Ikumbukwe siku chache kabla ya safari ya Cameroon, Mwamnyeto alipata msiba mkubwa wa kufiwa na mchumba wake kutokana na matatizo ya uzazi
Baada ya kurejea nchini kutoka Cameroon, Mwamnyeto alipewa muda zaidi wa mapumziko
Na sasa amerejea kazini kuipigania Yanga katika kampeni yake ya kuwania ubingwa wa ligi kuu
Anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri mkoani Mbeya siku ya kesho
ADVERTISE HERE