Kuhusu sakata la Ngoma, yaliyopita si ndwele tugange yajayo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Dec 2017
Kuhusu sakata la Ngoma, yaliyopita si ndwele tugange yajayo
Uongozi wa Yanga umemalizana 'kistaarabu' na mshambuliaji wake Donald Ngoma ambaye 'alitoroka' kambini na kwenda kwao Zimbabwe kujitibu majeraha yake.

Kitendo cha kuondoka bila ruhusa na kukaa kwao kwa zaidi ya wiki tatu kiliukera uongozi wa Yanga ulioapa kumchukulia hatua kali.

Hata hivyo utetezi ulioutoa umeweza 'kuulainisha' uongozi wa Yanga hivyo kumsamehe na kuachana na mpango wa kusaka mbadala wake.

Awali Ngoma alikuwa amezuiwa kufanya mazoezi na kikosi cha Yanga lakini kuanzia juzi, ameruhusiwa kurejea kambini sasa akijifua na mazoezi ya Gym mbioni kurejea dimbani.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ngoma kuwa kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga. Mwaka jana Ngoma aliingia kwenye marumbano na watalaamu wa tiba wa klabu ya Yanga akitilia shaka uwezo wao.

Wakati huo akitibiwa majeraha ya goti Ngoma alilalamika kutoridhishwa na matibabu hayo hivyo kumlazimu kutimkia Afrika Kusini.

Kinyume na anavyodhaniwa na wengi,Ngoma anapenda sana kuwa fiti muda wote kwa kuwa ni mchezaji anayependa kucheza mpira.

Moja ya sababu zilizompeleka Zimbabwe bila shaka ni kutibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kuitumikia Yanga kwenye michezo mitatu tu msimu huu.

Bila shaka wengi tunakumbuka jinsi Ngoma alivyokuwa akijituma katika michezo hiyo licha ya kuonekana akiugulia maumivu mara kwa mara.

Ngoma ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa katika kikosi cha Yanga bila shaka analifahamu hilo na hatopenda kukitia mchanga 'kitumbua chake'.

Inaelezwa kuwa baada ya kuona matibabu yake yanachukua muda mrefu Ngoma alimuomba ruhusa kocha Lwandamina ili akatibiwe kwao kwani aliamini wapo madaktari ambao wataweza kumrudisha dimbani mapema zaidi.

Na Pengine msimamo wake juu ya madaktari wa Yanga bado haujabadilika.

Hakuna shaka juu ya uwezo wa mshambuliaji huyu. Ndio, msimu huu hakuuanza vizuri lakini si yeye peke yake.

Amefunga mabao mawili katika michezo mitatu.

Kikosi kizima cha Yanga kilianza kwa kusuasua lakini baada ya michezo kadhaa ambapo yeye akiwa tayari ni majeruhi Yanga ilirejea katika kiwango chake.

Nina imani atakaporejea dimbani ataweza kuisaidia Yanga kama alivyofanya misimu miwili iliyopita wakati alipojiunga nayo akitokea Platinum FC ya Zimbabwe.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’