Mpaka sasa Yanga ndio timu bora zaidi katika ligi kuu ya Vodacom msimu huu wakikaa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama zao 44
Ubora wao unatokana na uimara wa safu ya ulinzi, utaona Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu
Maboresho yaliyofanyika katika usajili wa dirisha dogo yalilelanga kwenye safu ya ushambuliaji zaidi pamoja na kuwa Kocha Cedric Kaze pia aliongeza mlinzi wa kati Dickson Job ambaye pia ni kiraka anayeweza kucheza nafasi zote za ulinzi pamoja na kiungo
Nyota Saido Ntibazonkiza na Fiston Abdul Razak wamekuja kwa kazi moja tu, kuongeza idadi ya mabao
Kutokana na ushindani uliopo, yawezekana mabao yakahusika katika kuamua nani anakuwa bingwa
Hapa utaona mpaka sasa Simba wananufaika kwani wao wamefunga idadi kubwa ya mabao ukilinganisha na Yanga
Tofauti ya mabao kati ya Yanga na Simba mpaka sasa ni mabao 10, hivyo utaona safu ya ushambuliaji ya Yanga ina kazi ya kufanya katika michezo 16 iliyobaki
Kazi hiyo wanaianza Februari 13 katika mchezo dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa kule mkoani Mbeya. Kipaumbele cha kwanza ni ushindi lakini cha pili ni idadi ya mabao
Ni wazi mechi zilizosalia ushindani utakuwa mkubwa hivyo kwa zile mechi ambazo timu inapata nafasi ya kufunga mabao mengi inapaswa wafanye hivyo