Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza amesema timu imeimarika zaidi na wana matumaini makubwa katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Ntibazonkiza aliyetua Yanga katka usajili wa dirisha dogo, amesema kila mchezaji anafahamu malengo ya timu, ni jukumu lao kupambana kuhakikisha wanakamilisha malengo hayo
"Timu imeimarika sana, nafikiri ni zaidi ya vile nilivyokuwa nikiwaona kwenye TV kabla sijaanza kucheza. Kila mchezaji anajituma, wote tuna lengo moja tu, tunapambana kuutafuta ubingwa, inshallah Mwenye ez Mungu atatusaidia kufanikisha," Ntibazonkiza aliwaambia Wanahabari kwenye tukio la Wananchi Media Day
Aidha Ntibazonkiza amesema usajili wa mshambuliaji Fiston Abdul Razak umefanywa wakati sahihi na anaamini mchezaji huyo atakuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha Yanga katika duru ya pili ligi kuu ya Vodacom
"Nimemfahamu Fiston kwa miaka mingi, tumekuwa nae katika timu ya Taifa, ni mchezaji hatari kama hatakumbwa na changamoto ya majeraha, nafikiri mashabiki wajiandae kushangilia kila watakapomuona yuko uwanjani"
Ntibazonkiza amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua
Nyota huyo kwenye maandalizi ya kikosi cha Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa Februari 13 uwanja wa Sokoine