Mshambuliaji Amissi Tambwe amerejea kikamilifu mazoezi na bila shaka amepona kabisa majeraha ya goti yaliyomuweka nje tangu mwanzo wa msimu.
Tambwe ameanza kujifua kikamilifu na kikosi cha Yanga jana siku chache tangu arejee kutoka kwao nchini Burundi ambapo alipewa ruhusa kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia.
Kurejea kwa Tambwe kumeimarisha safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo katika michezo 9 iliyopita ya ligi imekuwa ikiwategemea washambuliaji wawili Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa baada ya Donald Ngoma kupata majeraha na kisha kuondoka kambini.
Ngoma nae tayari amesharejea nchini na uongozi wa Yanga umeamua kumbakisha kikosini hivyo kumaliza tetesi zilizoibuliwa awali kuwa mchezaji huyo alikuwa hatarini kuonyeshwa mlango wa kutokea.
Ngoma anaendelea na program binafsi ya mazoezi mpaka pale atakapokuwa tayari kurejea dimbani mwanzoni mwa Januari, 2018.

ADVERTISE HERE