Ukarabati wa vyumba Jangwani kuanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2021
Ukarabati wa vyumba Jangwani kuanza

Baada ya Yanga Elite kukamilisha zoezi la kupaka rangi jengo la klabu ya Yanga lililoko Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam, uongozi wa Yanga umeyataka Matawi mengine kujitokeza katika awamu ya pili ya ukarabati wa vyumba na miundombinu mingine ya jengo hilo

Afisa Habari wa Yanga amesema Yanga ni timu ya Wananchi hivyo kila Mwanayanga anapaswa kushiriki katika ujenzi wa timu hiyo kwani wao ndio wawekezaji wa klabu

Jengo hilo lina vyumba 30 ambapo Bumbuli amesema baada ya ukarabati kukamilika kikosi cha Yanga Princess kitaweza kuweka kambi hapo Jangwani

"Tumeanza kufanya tathmini ya gharama zinazohitajika kwa ajili ya ukarabati wa vyumba pamoja na ofisi, zoezi hilo litakapokamilika Wanayanga watajulishwa na kama walivyofanya Elite Group ambao wamegharamia zoezi lote la kulipaka rangi jengo, tunawaomba na Wanayanga wengine wajitokeze kugharamia ukarabati huo"

"Yanga ni timu ya Wananchi, Wawekezaji ni sisi wenyewe hivyo Matawi yote pamoja na makundi ya mitandao ya kijamii tuhamasishane kuhakikisha tunalikamilisha zoezi hili ili timu yetu ya Wanawake iwe na sehemu nzuri ya kuweka kambi," alisema Bumbuli

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’