Yanga yafafanua kuondoka kwa Mwambusi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2021
Yanga yafafanua kuondoka kwa Mwambusi

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amesema Kocha Msaidizi wa timu hiyo Juma Mwambusi aliandika barua akiomba apumzike kutokana na matatizo ya kiafya wakati kikosi cha Yanga kiko visiwani Zanzibar kikishiriki michuano ya kombe la Mapinduzi

Dk Msolla amesema Mwambusi aliomba kupumzika hivyo anaweza kurejea pale afya yako itakapokuwa imetengemaa

"Mwalimu Mwambusi aliandika barua rasmi wakati tuko Zanzibar kuomba apumzike kufuatia changamoto za kiafya"

"Kutokana na ushauri aliopewa na daktari, ametakiwa asiwe kwenye msongo wowote na asipige kelele wala kutumia sauti kubwa hata kwenye michuano ya Mapinduzi hakuwa anazungumza kwa sauti kubwa"

"Hivyo tumemruhusu apumzike, hata Wachezaji wanaugua wakipona wanarejea kwahiyo hata yeye akipona atarejea," alisema Dk Msolla

Aidha Dk Msolla amefafanua tetesi zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanakusudia kumuajiri kocha wa African Lyon Nizar Khalfan kuchukua nafasi ya Mwambusi

"Hilo suala la Nizar Khaflan kuchukua nafasi ya Mwambusi itategemea na matakwa ya Mwalimu kwa sababu yeye ndiye alimpendekeza Mwambusi mwanzo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’