Tunaanza kuhesabu mataji leo - Mwakalebela

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jan 2021
Tunaanza kuhesabu mataji leo - Mwakalebela

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema leo hawatakuwa na 'simile' kwenye mchezo wa fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya watani zao Simba kwani wanahitaji kuanza kuhesabu mataji

Akizungumza kutoka visiwani Zanzibar mapema leo, Mwakalebela amesema wamefurahi mchezo wa fainali kuwakutanisha na watani zao kwani walihitaji nafasi hii kudhihirisha ubora wao

"Tumefurahi mchezo wa fainali tunacheza na watani zetu Simba, tulikuwa tukiwawinda kwelikweli hatimaye wameingia kwenye anga zetu. Viongozi tumezungumza na wachezaji kuwaeleza umuhimu wa kushinda leo na kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi. Wametuahidi, wako tayari kufia uwanjani ili mradi tu wahakikishe tunashinda ubingwa leo"

"Kwa misimu mitatu timu yetu haikushinda kikombe chochote hivyo leo tumepania kuanza kuhesabu mataji ya msimu huu. Tunaanza na hili la Mapinduzi, kisha ligi kuu na kombe la FA"

"Mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kuwapa hamasa wachezaji wetu, nawaambia leo watarudi nyumbani wakiwa na furaha," alisema Mwakalebela

Mpaka kufikia saa kumi jioni uwanja wa Amaan tayari umefurika mashabiki kuelekea mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa mbili na robo usiku

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’