Spana ya Mwakalebela inavyomtesa Morrison

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Jan 2021
Spana ya Mwakalebela inavyomtesa Morrison

Hivi karibuni uongozi wa Simba ulidai kuwa Benard Morrison hakuwa akionekana katika kikosi cha timu hiyo kwa kuwa ni mgonjwa

Lakini Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alifichua kuwa mchezaji huyo amepigwa stop na Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS) akisubiri kusikilizwa kwa shauri lake dhidi ya Yanga Januari 12

Jana Morrison alionekana jukwaani wakati timu ya Simba ikicheza na Fc Platinum. Ni tukio lililodhihirisha kauli aliyotoa Mwakalebela baada ya Ismail Aden Rage aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba kudai kuwa uongozi wa Yanga umewahadaa wanachama na mashabiki wake kuwa hakuna kesi waliyofungua CAS

Mwakalebela alisema hatma ya kesi waliyofungua dhidi ya mchezaji huyo itafahamika baada ya kupangiwa Jaji ambaye anaanza kuisikiliza Januari 12

Yanga inapinga hukumu iliyotolewa na kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kubatilisha mkataba wa Morrison na Yanga na kumruhusu mchezaji huyo ajiunge na Simba

Morrison alipewa nafasi ya kujitetea na CAS lakini utetezi wake ukaonekana hauna mashiko na hivyo kesi hiyo kupangiwa Jaji wa kuisikiliza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’