Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana jana dhidi ya Jamhuri Fc, Yanga imewekeza katika mchezo wake wa pili dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa keshokutwa Ijumaa
Matokeo ya ushindi yataihakikishia Yanga kusonga mbele hatua inayofuata ya michuano ya kombe la Mapinduzi
Jana kocha Cedric Kaze alianza na kikosi kilichosheheni wachezaji wengi ambao hawachezi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, Ijumaa anatarajiwa kuingia kivingine
Nyota kama Saido Ntibazonkiza ambaye jana hakuvaa kabisa jezi, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Namungo Fc
Msimu huu Yanga imepania kufanya vizuri katika kila mashindano wanayoshiriki bila ya kujali ukubwa wa mashindano hayo
Misimu ya nyuma Yanga ilikuwa na kawaida ya kutumia kikosi cha pili katika michuano hii lakini msimu huu wameonyesha dhamira kwani Kaze alisafiri na wachezaji wake wote 20 ambao wako kikosini wakati huu