Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza Januari 05 2021, Yanga ikipangwa kundi A sambamba na timu za Namungo Fc na Jamhuri kutoka Pemba
Mchezo wa kwanza wa Yanga ni dhidi ya Jamhuri, Januari 05 ukipigwa saa mbili na robo usiku, uwanja wa Amaan
Yanga itashuka tena dimbani Januari 08 kucheza na Namungo ukiwa ni mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi
Aidha, kundi B litakuwa na timu za Mtibwa Sugar, Simba na Chipukizi wakati kundi C litakuwa na timu za Azam Fc, Malindi na Mlandege Fc

ADVERTISE HERE