Kumbe Wakili kapigwa spana na CAS

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2020
Kumbe Wakili kapigwa spana na CAS

Kwa takribani wiki mbili winga Bernard Morrison hachezi kwenye kikosi cha Simba uongozi wa klabu hiyo ukidai kuwa Mghana huyo ni mgonjwa

Lakini imebainika kuwa rufaa ambayo Yanga walikata kule Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) imeanza kusikilizwa na mchezaji huyo amezuiwa kuitumikia Simba hadi pale shauri lake litakapokamilka

Kulingana na gazeti la Sport Xtra, ni zaidi ya wiki moja na nusu imepita tangu Simba wapokee barua hiyo kutoka CAS ikiwataka wasimtumie Morrison kutokana na shauri lililofunguliwa na Yanga

Morrison anaweza kuingiza Simba matatani na hata TFF kama CAS itapindua hukumu iliyotolewa na Kamati Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ilibatilisha mkataba wake na klabu ya Yanga na kumruhusu ajiunge na Simba akiwa mchezaji huru

Simba pia inakabiliwa na kesi nyingine ya usajili wa Shiza Kichuya ambapo klabu ya Pharco Fc iliituhumu Simba kumsajili mchezaji huyo bila ya kufuata utaratibu

Awali FIFA ilitoa hukumu kwa kuitaka Simba ilipe faini inayofikia Tsh Milioni 300 au la itafungiwa kusajili kwa misimu mitatu

Simba iliomba mapitio ya hukumu hiyo ambayo ndiyo yamemfanya Kichuye aruhusiwe kuendelea kucheza kwani tayari alikuwa amefungiwa miezi sita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’