Majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata Kelvin Yondani jana kwenye michuano ya Cjalenji kati ya Kilimanjaro Stars dhidi ya Zanzibar Heroes, yatamuweka nje kwa wiki mbili.
Daktari wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Dk Richard Yomba amesema Yondani tayari ameanza matibabu na atakuwa kamili kurejea dimbani baada ya wiki mbili.
Hii ni habari njema kwa Yanga kwani sasa atakuwa tayari kuchuka dimbani kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12 dhidi ya Mbao FC, Disemba 29.
Yondani huenda akakosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Reha utakaopigwa kati ya Disemba 20 na 25.

ADVERTISE HERE