Kwa takribani wiki nzima jina la mshambuliaji Mnyarwanda Jacquis Tuyisenge limetajwa sana akihusishwa na Yanga
Tuyisenge alijiunga na APR katika usajili uliopita akitokea klabu ya Petro ya Angola
Tuisenge ni mchezaji mwenye uzoefu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Kabla ya kutimkia Angola, aliwahi kuichezea klabu ya Gor Mahia akicheza na wachezaji kama Meddie Kagere, Joash Onyango na Francis Kahata ambao wote walisajiliwa na Simba
Mwezi Julai, Tuyisenge alitajwa kukaribia kutua Yanga lakini dili lake lilishindikana dakika za mwishoni
Inafahamika katika kipindi hiki cha dirisha dogo, Yanga itaimarisha safu yake ya ushambuliaji, wakitajwa kuwa mbioni kusajili mshambuliaji wa kati (namba 9)
Juzi Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alidokeza kuwa wako mbioni kukamilisha usajili wa mchezaji matata ambaye atakuja kuongeza ubora kwenye safu ya ushambuliaji
Je ni yeye? tusubiri...