Shoo ya Ntibazonkiza inasubiriwa Arusha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2020
Shoo ya Ntibazonkiza inasubiriwa Arusha

Ni uhakika Yanga itaweza kumtumia mshambuliaji wake mpya Saido Ntibazonkiza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa kesho Jumamosi uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha

Yanga imekamilisha vibali vya mchezaji huyo wakati TFF ikitarajiwa kutoa leseni kumuwezesha kushuka dimbani hapo kesho

Nyota wa Yanga akiwemo Ntibazonkiza wamekuwa gumzo kwa mashabiki mkoani Arusha kuelekea mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hapo kesho Jumamosi

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema anaamini nyota huyo raia wa Burundi ataongeza ubunifu na uzoefu wake utakuwa msaada mkubwa katika kikosi chake

Juzi baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United, Kaze alieleza kuridhishwa na kiwango alichoonyesha Ntibazonkiza akimsifu kuwa amefanya kile ambacho kila mmoja alikitarajia kutoka kwake

Katika mchezo huo uliokuwa wa kwanza kuitumikia Yanga, Ntibazonkiza alifunga mabao mawili

"Ni mchezaji mzuri ameonesha kile tulichotarajia, anajua kuchezesha timu na kuongoza wenzake uwanjani," alisema Kaze

Mwenyewe Ntibazonkiza amesema amekuja kutumia uzoefu wake kuisaidia Yanga akishirikiana na wanachezaji wenzake kuhakikishia watafikia malengo yaliyokusudiwa ya kutwaa ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’