Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa Jumatano, uongozi wa klabu ya Yanga unatarajiwa kuweka hadharani majina ya wachezaji watakaotolewa kwa mkopo
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema yapo majina ya wachezaji ambao amependekeza watolewe kwa mkopo ili wapate nafasi zaidi ya kucheza
Amesema majina ya wachezaji hao yatatolewa na kitengo cha habari cha klabu ya Yanga
Aidha kuhusu usajili dirisha dogo, Kaze amesema watakutana na uongozi kujadiliana, kama wataona kuna umuhimu wa kuongeza mchezaji basi watasajili
Hata hivyo Kaze amesisitiza kuwa mchezaji atakayesajiliwa na Yanga kwenye dirisha hilo ni lazima awe bora zaidi ya wachezaji waliopo
Yanga tayari imesajili mchezaji mmoja Saido Ntibazonkiza ambaye ataanza kuwatumikia Wananchi wiki ijayo