Wakati kaka zao wakitoa adhabu kali mkoani Shinyanga kwa kuwafumua Mwadui Fc mabao 5-0, kinadada wa Yanga Princess wamewakomalia watani zao Simba Queens wakiwalazimisha suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake ambao ulipigwa uwanja wa Mo Arena
Haya ni matokea muhimu sana kwa Yanga Princess ambayo misimu iliyopita haikuwa imara hivyo kupoteza mechi zote dhidi ya Simba Queens tena kwa idadi kubwa ya mabao
Kwa hakika viongozi wa Yanga wanastahili pongezi kwa uwekezaji waliofanya katika timu hiyo ya Wanawake
Mpaka sasa haijaruhusu bao kwenye nyavu zake katika mechi nne walizocheza
Msimu huu Wananchi wana jambo lao, hawaachi kitu..!
ADVERTISE HERE