Yanga yawanyemelea Juuko, Mzamiru

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2017
Yanga yawanyemelea Juuko, Mzamiru
Wachezaji wawili wa Simba, kiungo Mzamiru Yassini na beki Juuko Murshidi wako mwishoni mwa muda wa mikataba yao na klabu hiyo.

Wachezaji hao mikataba yao imebaki chini ya miezi sita hivyo wanaruhusiwa kufanya mazungumzo ya awali na timu yoyote.

Mzamiru anaweza kuwa mbadala sahihi wa Thabani Kamusoko kama kiungo huyo raia wa Zimbabwe anayetibiwa majeraha ya goti atashindwa kupona kwa wakati.

Ikumbukwe Yanga inakabiliwa na michuano ya klabu bingwa barani Afrika na michuano hiyo ndio kipaumbele cha kwanza msimu huu.

Hivyo inahitaji kuingia kwenye michuano hiyo ikiwa na kikosi kamilifu.

Juuko Murshidi ni beki mzoefu. Amecheza mechi nyingi za Kimataifa akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda Cranes.

Ana bahati mbaya tu haaminiwi na kocha wa Simba Joseph Omog lakini uzoefu wake si wakutiliwa shaka hata kidogo.

Kwa timu inayoshiriki michuano ya kimataifa, huyu ni mtu sahihi kuwa nae.

Hata hivyo kama Yanga itafanikiwa kufikia nao makubaliano, wachezaji hawa watatua baada ya mikataba yao na Simba kumalizika.

Yanga na Simba haziuziani wachezaji wenye mikataba hai!

Vita ya kupokana wachezaji baina ya Yanga na Simba haijaanza leo na haitakwisha.

Jambo hili halipendwi na mashabiki hasa wale wa timu inayopoteza mchezaji lakini kwa mchezaji ni neema kwake.

Mchezaji kazi yake ni kusakata soka hivyo hawezi kukataa kuhamia sehemu yenye maslahi zaidi kuliko hapo alipo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’