Mlandizi Queens wamekutana na tiki-taka la Yanga Princess huko Mabatini Pwani baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa vinara hao wa ligi kuu ya Wanawake
Aisha Masaka ameendelea kuwakimbiza akifikisha mabao sita leo baada ya kutupia tena
Fatuma Mwisendi ndiye aliyeihakikishia Yanga Princess ushindi muhimu kwa bao lake la dakika ya 75
Yanga Princess wanaendelea kusimama kileleni mwa msimamo wa ligi wakijikusanyia alama tisa na mabao 11
jambo jema zaidi mpaka sasa nyavu za Yanga Princess ziko salama hawajaruhusu bao hata moja
Wananchi wanamaanisha, msimu huu 'wanasepa' na mataji yote
ADVERTISE HERE