Kaze awapa neno washambuliaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Dec 2020
Kaze awapa neno washambuliaji Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema ameona mabadiliko katika safu yake ya ushambuliaji na kumtaka mshambuliaji wake, Mghana Michael Sarpong, kuendeleza kasi yake ya kupambana kuhakikisha anaendeleza spidi ya kufunga kila anapompa nafasi ya kucheza

Hatua hiyo imekuja baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, huku Sarpong akifunga la kwanza dakika ya 30 na kufikisha mabao manne kwenye Ligi Kuu hadi sasa

Kaze alisema kufunga kwa Sarpong katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting bado hawezi kuweka wazi kwamba safu yake ya ushambuliaji iko vizuri, hivyo anamtaka kupambana zaidi, huku akiongeza umakini na utulivu anapokuwa uwanjani.

Alisema ilikuwa mechi ngumu kutokana na timu waliyocheza nayo kufundishwa na kocha mzoefu, lakini tatizo kikosi chake kimekuwa kikitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.

"Sarpong amefunga amefikisha mabao manne hayupo mbali na anayeongoza katika ufungaji ambaye ana mabao saba, lakini sitahesabu kwamba safu ya ushambuliaji imekuwa na mabadiliko makubwa bali anapaswa kuendelea kufunga kila mechi,” alisema Kaze

Alisema anaendelea kuwasisitizia washambuliaji wake kuwa watulivu wanapokuwa uwanjani, ambapo tayari amefanikiwa katika nafasi zingine ikiwamo ya ulinzi, viungo pamoja na mawinga ambao walifanya kazi nzuri katika michezo mitatu iliyopita.

"Wachezaji wangu wanafuata maelekezo ndani ya uwanja jambo linalowafanya wanapata matokeo chanya, lakini kutumia vema makosa wa wapinzani kuwa faida kwetu," alisema Kaze.

Alisema hatua ya kumuita Deus Kaseke baada ya kukosa mkwaju wa penalti, lengo kubwa lilikuwa kumtuliza na kumtaka asahau makosa hayo.

Kuhusu ujio wa Saidi Ntibazonkiza, alisema ni mchezaji mzuri na atakuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa sababu anafahamu uwezo wake pamoja na uzoefu alionao katika soka.

"Ni mchezaji mzuri, ana uzoefu mkubwa kwa sababu amecheza soka Ulaya muda mrefu, ataongeza nguvu na uzoefu aliokuwa nao kwa wachezaji ambao wapo hapa, suala la ufungaji nina imani bado nitaendelea kuwapa mbinu mpya ili tutoke katika kupata bao 1-0" alisema kocha huyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’