Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze ameeleza kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao umewashuhudia wananchi waiondoka na alama zote tatu kwa ushindi wa mabao 2-1
Kaze amesema alifahamu watakabiliwa na mchezo wa nguvu kutoka kwa Ruvu Shooting hivyo aliwaandaa wachezaji wake kimbinu na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuwadhibi wapinzani wao
"Tulijua tunaenda kukutana na timu yenye nguvu , wako haraka kushambulia tulijiandaa kuwakabili," alisema Kaze
"Tulikuwa na nafasi ya kumaliza mchezo mapema lakini bahati haikuwa upande wetu tukakosa penati"
"Binafsi nimefurahishwa na kiwango cha timu yangu siku ya leo, japo kuna marekebisho ambapo tutarejea imara zaidi mchezo ujao kwa kuyafanyia kazi mapungufu ya mchezo wa leo"
Yanga ilikuwa bora sana katika mchezo huo ambao ilifunga mabao yake kupitia kwa Michael Sarpong na mlinzi wa Ruvu Shootinga Castian Ponera akijifunga