Pumzika kwa amani Joel Nkaya Bendera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2017
Pumzika kwa amani Joel Nkaya Bendera
Kocha aliyeiwezesha Tanzania kufuzu fainali pekee za Kombe la soka la Mataifa ya Afrika (AFCON), Joel Nkaya Bendera amefariki dunia jioni ya leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Msemaji wa hospital ya Muhimbili, Aminieli Eligaisha ameithibitisha kufariki kwa Bendera aliyewahi pia kuwa Naibu Waziri wa Michezo wakati wa Serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Bendera ambaye Mei 30, mwaka huu amefikisha umri wa miaka 67, umaarufu wake ulianza akiwa kocha wa mpira wa miguu na alikuwa kocha wa timu ya taifa iliyofanikiwa kuitoa Zambia mwaka 1979 na kukata ya Fainali za AFCON mwaka 1980 nchini Nigeria.

Bendera akaendelea kuwa kocha miaka ya 1980 kabla ya kustaafu na kuhamia kwenye siasa ambako alianzia kwa kugombea ubunge wa jimbo la Korogwe mkoani Tanga mwaka 1995 na akafanikiwa kushinda.

Bendera alilishikilia jimbo hilo hadi mwaka 2010 alipoangushwa kwenye kura za maoni za CCM na Abdallah Nassir Yussuf kwa tofauti ya kura 255 tu.

Akiwa Mbunge wa Korogwe, Bendera pia alikuwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo tangu mwaka 2006 hadi 2010.

Na ni kipindi hicho ambacho Tanzania ilipata tiketi ya kucheza Fainali za michuano mingine mikubwa Afrika, CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast, michuano inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.

Baada ya hapo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Manyara, ambao umekuwa kituo chake cha mwisho cha utumishi wa umma kabla ya kukutwa na umauti.

Bendera alikuwa mpenzi wa michezo enzi za uhai wake hususan soka na aliendelea kujihusisha na mchezo hadi siku za mwisho za uhai wake, akishiriki kuhamaisha michezo kwa watoto.

Taifa limempoteza mtu muhimu katika sekta ya michezo. Ni pengo ambalo haliwezi kuzibika milele. Anaondoka na rekodi yake pekee ya kukumbukwa milele.

Mwalimu pekee aliyeweesha Taifa Stars kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mungu ampumzishe kwa amani Mwalimu Joel Nkaya Bendera. Amin.

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
58m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’