Kaze afafanua uchovu wa wachezaji kipindi cha pili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Nov 2020
Kaze afafanua uchovu wa wachezaji kipindi cha pili

Jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania, Yanga ilikuwa bora sana kwenye kipindi cha kwanza

Ni katika kipindi hicho ilijipatia bao pekee lililowapa alama tatu kupitia kwa Deus Kaseke

Kipindi cha pili mabingwa hao wa kihistoria walipunguza kasi wakiwapa JKT Tanzania nafasi ya kurejea mchezoni na kutengeneza mashambulizi mengi langoni kwa Yanga

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze ameeleza kuwa hali hiyo ilitokana na uchovu wa wachezaji baada ya kucheza mfululizo pasipo kupata muda wa kutosha wa kupumzika

"Leo ni siku ya nane, tumecheza mechi tatu ndani ya kipindi hiki. Wachezaji asilimia kubwa ni hawahawa waliocheza mechi hizo. Ni wazi tumeathiriwa na uchovu," alisema Kaze

Aidha,  Kaze alieleza kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake kwenye kipindi cha kwanza lakini hakufurahishwa na nafasi nyingi walizotengeneza hawakuzitumia

Mchezo unaofuata wa Yanga ni Disemba 06 dhidi ya Ruvu Shooting vijana wa Charles Mkwasa ambao msimu huu wako moto kwelikweli

Angalau wachezaji watapata wiki moja ya kujiandaa na mchezo huo, bila shaka pia watarejea wakiwa hawana uchovu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
32m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
41m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’