FT : Azam Fc 0-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2020
FT : Azam Fc 0-1 Yanga

Yanga imepanda kileleni mwa msimamo wa ligi kibabe baada ya kuichapa Azam Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Huu ni ushindi wa kibingwa kwa Yanga, kwani wameondoka na alama tatu dhidi ya wapinzani wao Azam Fc ambao hatimaye wameachia usukani wa ligi baada ya kuongoza kwa muda mrefu

Ni mchezo ambao kocha Cedric Kaze alifanikiwa kimbinu, kwani Yanga ilikuwa hatari sana kila iliposhika mpira

Bao pekee la ushindi liliwekwa kambani na kiraka Deus Kaseke 'Deda 04' aliyemalizia vyema pasi murua ya Yacouba Sogne

Mpira ulianzia kwa Ditram Nchimbi aliyemsetia Yacouba pasi maridhawa naye kumuwekea katika njia Kaseke

Yanga ilikuwa imara zaidi leo eneo la kiungo pamoja na safu ya ulinzi wakifanikiwa kuwadhibiti kabisa Azam Fc ambao walizinduka katika kipindi cha pili

Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe alama 28 sasa ikikaa kileleni kihalali kwa tofauti ya alama tatu dhidi ya Azam Fc na alama tano dhidi ya Simba

Ni mwendo wa rekodi kwa kocha Kaze kwani kikosi chake hakijapoteza mchezo wowote msimu huu

Yaani Yanga haijafungwa kabisa iwe kweye ligi au mchezo wa kirafiki

Wananchi wana kila sababu ya kutamba kwani msimu huu unaweza kuwa na furaha kwao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’