Kaze kutumia dirisha dogo kuimarisha kikosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Nov 2020
Kaze kutumia dirisha dogo kuimarisha kikosi

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amekiri kuwa kikosi chake bado kina changamoto kwenye baadhi ya maeneo na atatumia dirisha dogo la usajili kukiimarisha

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa wiki tatu zijazo Yanga ikiwa tayari na uhakika ya huduma ya kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ambaye alisajiliwa mwezi uliopita

Akizungumza juzi baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1, Kaze alibainisha mapungufu aliyoyaona

Hata hivyo akasisitiza kuwa kwa sasa bado hawawezi kuzungumzia ni maboresho gani watayafanya, muhimu ni kusubiri dirisha dogo litakapofunguliwa mwezi ujao

"Naweza kusema yapo maeneo ambayo tutahitaji kuongeza nguvu, ila sitaweza kuweka wazi kwa sababu nitawavunja moyo wachezaji niliokuwa nao wakati bado tuna michezo sita kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa

"Ni kama tulikosa mwelekeo katika mechi tatu mfululizo tulizopata sare hivi karibuni. Tulifanya makosa ambayo yalitugharimu tusiweze kuondoka na ushindi, tumefanyia kazi changamoto hizo, tumejipanga kuhakikisha haturudii makosa mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc" alisema Kaze

Kesho Kaze atakuwa na nafasi nyingine ya kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi kama atafanikiwa kuondoka na ushindi dhidi ya Azam Fc

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’