Mshambuliaji Ibrahim Ajib Migomba 'fundi wa mpira' hataweza kucheza mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12 dhidi ya Mbao FC baada ya kutimiza kadi tatu za njano.
Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amethibitisha Ajib kuwa na kadi tatu za njano alizozipata kwenye michezo dhidi ya kagera Sugar, Simba na Prisons.
Licha ya kukosekana kwa mchezaji huyo aliyeifungia Yanga mabao matano, Yanga inao wachezaji wanaoweza kuziba nafasi yake kwa ufasaha.
Bila shaka Amissi Tambwe atakuwa timamu na tayari kurejea dimbani katika mchezo huo huku pia Yanga inaweza ikamtumia kinda aliyesajiliwa dirisha dogo la usajali, Yohana Nkomola.
Yanga pia iko mbioni kuongeza mshambuliaji mmoja wa Kimataifa kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa Disemba 15.

ADVERTISE HERE